
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk Bashiru Ally
KITETO
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk
Bashiru Ally amekemea vikali vitendo vya polisi kutumia mabavu
bila sababu ya msingi kwa ajili ya kushughulikia migogoro ya
7/13/2019 Dk Bashiru awaonya polisi kutotumia mabavu kushughulika na wanasiasa kisiasa.
Bashiru akizungumza jana Ijumaa Julai 12,2019 mji mdogo wa
Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara nchini Tanzania akiwa
kwenye ziara, alisema hakuna ulazima wa kutumia mabavu bila
sababu maalum.
Alisema mabavu yanapaswa kutumika kama yalivyotumika
kumpiga aliyekuwa Rais wa Uganda, Iddi Amin lakini wananchi
msivichokonoe na kuvichokoza vyombo vya dola.
"Tukianza kutumia mabavu katika kutatua migogoro yetu ni dalili
ya kushindwa kuongoza nchini kwani hakuna sababu ya kuyatumia
ili hali wananchi wanatii sheria bila shuruti,” alisema
Alimuagiza mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti
kuhakikisha vyombo vya ulinzi na usalama havitumii nguvu kubwa
bila sababu ya msingi kwani hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Alisema nguvu ya ziada inapaswa kuanza kutumika endapo
itaonekana kuwa bila mabavu mambo hayawezi kuwa sawa hadi
lifanyike jambo hilo.
"Namna tutakavyoona vyombo vyetu vya ulinzi na usalama
havitumii mabavu ndivyo tutakavyopima mfumo wetu wa kisiasa,
demokrasia na uongozi ulivyo na unavyofanya kazi vizuri," alisema
Dk Bashiru.
Hata hivyo, mkuu wa polisi wa wilaya ya Kiteto, Fadhili Luoga
alisema kwenye eneo lao hawajawahi kutumia mabavu kwenye
ulinzi katika shughuli za kisiasa.
"Chama chochote cha kisiasa kikitaka kufanya mkutano wake wa
hadhara kupitia madiwani au mbunge wanatoa taarifa kwetu na
tunawapa ulinzi na bila kuwepo na tatizo lolote hatuwezi kutumia
nguvu labda pale inapobidi," alisema Luoga.
Katibu wa chama cha NCCR-Mageuzi wilayani Kiteto, Christopher
Laizer alipongeza hatua hiyo kwani matukio ya askari polisi nchini
Tanzania kuwanyanyasa wapinzani bila sababu ya msingi imekuwa
ni kawaida.
"Pamoja na kuwa mimi ni mpinzani ninampongeza sana katibu
mkuu wa CCM kwa maneno yake ya kuwaasa polisi kuwa
wasitumie mabavu bila sababu ya maana," alisema Laizer.
Katibu mwenezi wa Chama cha Wananchi (CUF), Hassan
Mohamed alisema kauli kama hiyo ni ya kujenga demokrasia
kwani baadhi ya askari polisi nchini wamekuwa na mtindo wa
kuwanyanyasa wapinzani ikiwemo kuwapiga mabomu ya machozi.
Alisema polisi wanapaswa kukaa pembeni na kuwaachia CCM,
CUF, Chadema na vyama vingine vipambane jukwaani kwa hoja na
siyo kuingilia kati na kunyanyasa wapinzani kama wanavyofanya
sasa.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment