} });
 

Jambazi mmoja amefariki Dunia kwa kupigwa risasi na Polisi, baada ya kufanya tukio la uvamizi kwenye duka la kutoa huduma za kifedha Mtaa wa Msalala, Kata ya Kalangalala mkoani Geita, huku na yeye akijeruhi watu wawili kwa risasi, baada ya kuanza kurusha risasi hizo hovyo.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 13, 2020 na Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Geita ACP Mtatiro Kitinkwi, na kutaja jina la Jambazi huyo aliyeuawa kuwa ni Daniel Jacksoni, ambapo aliuawa baada ya kukaidi agizo la Polisi walilomtaka kujisalimisha.

 

"Baada ya Jambazi huyo kuwaona Askari alikimbia huku akirusha risasi hovyo na baada ya kurusha risasi hizo na alijeruhi raia wawili, na baadaye Askari walimtaka ajisalimishe lakini akakaidi, na wao hawakumchelewesha wakampiga risasi", amesema Kamanda Kitinkwi.

 

Aidha Jeshi hilo linashikilia Bunduki aina ya short gun 12 bore(pump action), yenye namba MV.97465X ambayo ilikuwa ikitumiwa na marehemu katika tukio hilo la ujambazi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top