} });
 

 

Chama cha The Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda kimejipata katika njia panda baada ya muasisi wa chama hicho na mgombea mara nne wa urais , Kizza Besigye, kukataa ombi la kupeperusha tena bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa ujao wa 2021.

 

Dkt Besigye, ambaye alipambana na Rais Museveni katika chaguzi nne za urais zilizopita tangu mwaka 2001, kila mara alimshutumu Rais huyo kuiba kura.

 

Alikwenda mara mbili katika Mahakama ya juu mwaka 2001 na 2006 na katika kesi zote hizo kwa kauli moja Majaji walithibitisha kuwa kulikua na wizi wa kura lakini kwa mgawanyiko wa kura mwaka 5:2 na 4:3 mwaka 2006 , huku wengi wa majaji wakiamua kuwa wizi wa kura haukutosha kubatilisha matokeo ya mwisho ya kura.

 

Uamuzi wa Dkt. Besigye wa kutogombea urais mwaka 2021 umekiacha Chama cha FDC kikimtafuta atakayekiwakilisha katika uchaguzi huo, ayari chama hicho kimeaihirisha mara mbili uteuzi wa wagombea wake wa uraiskwa matumaini kuwa Dkt. Besigye angebadili msimamo wake na kuchukua fomu za uteuzi.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top