} });
 


Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Democrat cha nchini Marekani Joe Biden amemteua Seneta wa Califonia Kamala Harris kuwa mgombea mwenza kwenye kinyang’anyiro hicho.

 

Aidha hatua hiyo inaandika historia mpya nchini Marekani kwa mwanamke huyo mweusi na raia wa kwanza mwenye asili ya Marekani na Asia kugombea nafasi yenye wadhifa wa juu katika kinyang’anyiro cha Urais.


 

Harris ameandika kupitia mtandao wake wa twitter baada ya kuteuliwa akisema anajisikia heshima kuungana na Biden na amekubali kufanya kila liwezekanalo kumsaidia kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

 

Harris alikuwa karibu na mtoto wa Biden Beau, aliyekuwa mwanasheria mkuu katika jimbo la Delaware na yeye akiwa na wadhifa kama huo katika jimbo la California.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top