} });
 

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Agosti 25, 2020 ametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kupita bila kupingwa katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Ruangwa.

Akitangaza matokeo hayo kwenye viwanja vya Osi ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Frank Chonya amesema Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Majaliwa ndiye pekee aliyekidhi vigezo vilivyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kumfanya kupita bila kupingwa.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa amepita bila kupingwa, Mheshimiwa Majaliwa amesema anawashukuru  wanaCCM, Viongozi na  wanachama wa vyama raki  na wana Ruangwa kwa ujumla kwa heshima waliyompatia na kumwezesha kupita bila kupingwa. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top