} });
 

 

Aliyekuwa Meneja wa msanii Rich Mavoko, Meneja Maneno amesema waliwahi kwenda kwa mganga wa kienyeji na msanii huyo kwa ajili ya kutumia mbinu za kuweza kupita ili kutoboa katika maisha ila sasa hivi hategemei kufanya hivyo tena. 

"Kwa Mganga tulienda kwa sababu zile zilikuwa mbinu za njia za kupita ili kuweza kufanikiwa, usitegemee kutuona tena kwa waganga ila tegemeeni  kuona muunganiko mzuri kwetu na kumuona Rich Mavoko anakwenda sehemu nzuri, mambo mengine yote yamepita na tumeweza kusuluhisha" amesema Meneja Maneno

 

Pia Meneja Maneno ameongeza kusema kuna muda alikuwa amepaniki hali ambayo ilipelekea kuwa na tofauti kati yao na ilipita muda wa miaka 6 bila ya kuzungumza japo walikuwa wanakutana kwenye shughuli za kisanii.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top