} });
 

 

WATU watatu wamekamatwa na kushitakiwa kutokana na kuhusika kujaribu kuwapa rushwa  na kuwatishia maisha wanawake ambao walimshitaki R. KELLY kwenye kesi yake inayomkabili ya unyanyasaji wa kijinsia.

 

Kwa mujibu wa NBC News New York, watu hao wanaohisiwa kuwa na ukaribu na nguli huyo wa R&B walijaribu kutega kitu chenye asili ya bomu katika gari la baba wa mmoja wa wanawake ambao wamemshitaki R. Kelly.

 

Shitaka hilo lililofunguliwa na mwanasheria wa wanawake hao , limewataja watu hao kuwa ni Richard Airlines, Donnell Russell na Michael Williams ambao wote wana uhusiano wa karibu na mwanamuziki huyo.

 

“Kwa vitu walivyojaribu kuvifanya watu hawa, inaonyesha wazi kuwa wanaweza kufanya tukio lolote bila hofu ili kumsaidia R. Kelly katika kesi hii,” aliongea wakili Peter Fitzhugh.

 

Licha ya ushahidi mkubwa kuthibitisha kuwa Kelly alihusika katika makosa mbalimbali ya unyanyasaji wa kijinsia, lakini mpaka hivi sasa  ameendelea kukana mashitaka yote yanayomkabili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top