} });
 

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina mapema leo amekitembelea kiwanda cha Gereza Kuu la Karanga ambacho kinatarajiwa kuanza kuzalisha viatu pamoja na bidhaa nyinginezo za ngozi kuanzia Oktoba Mosi, kilichogharimu zaidi ya Shilingi billion 69.

Akiwa kiwandani hapo, Waziri Mpina amesema kuwa Serikali imeamua kuja na majibu kutokana na maswali ya wananchi waliokuwa wakihoji kuhusu wapi kwa kupeleka malighafi ya ngozi za wanyama wanazozizalisha kwa muda mrefu hivi sasa.

 

''Swali hili linaulizwa na wananchi wengi, serikali hatukuwa na majibu, wananchi wanazalisha ngozi kule. Tuanatambua kuwa nchi yetu inamifugo mingi na ni ya pili Afrika lakini wanazalisha ngozi hawana mahala pa kuziuza, sasa serikali ya awamu ya tano ndipo ilipo amua kwa makusudi kuhakikisha kwamba kiwanda hiki kijengwe'', amesema Waziri Mpina.

 

Aidha Luhaga Mpina amekitaka kiwanda hicho kutoa kipaumbele kwa ngozi za wafugaji wa ndani, na kuongeza kuwa ngozi za nje zitaagizwa kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo, pia Waziri amewataka wafugaji kutunza vyema mifugo yao katika namna ambayo itafanya mifugo huyo kutoa ngozi zenye ubora ili kukidhi viwango vya ngozi zinazohitajika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi.

 

Imeelezwa kuwa kwa sasa Tanzania inaagiza zaidi ya pea milioni 50 za viatu huku uzalisahaji wa ndani ukiwa ni pea milioni 1.6, kwa upande wa ngozi zinazozalishwa nchini ni milioni 11.5, ngozi za ng'ombe million 4.5, mbuzi milioni 4.6 huku ngozi za kondoo zikiwa ni milioni 1.6, uchakataji wa ngozi hizo za ng'ombe ni 170,000, za mbuzi ni 720,000.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top