} });
 

 

Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia wahamiaji haramu (Wanaume) ,kutoka nchini Ethiopia wapatao 51 kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. 

Kamanda wa Polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa amethibitisha juu ya tukio hilo ambapo amesema “katika eneo la Mzani wa magari Msata Chalinze Polisi wakiwa doria barabara kuu ya Chalinze kuelekea Tanga walikamata gari namba T.246 BBG aina ya scania tani 10 hard top” 

Alieleza gari hilo lilipopekuliwa lilikutwa likiwa na raia 51 wote wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 15-25 ambao walikuwa wanasafirishwa kutoka Tanga -kuelekea Chalinze kupitia Msata na watu wawili wanaodhaniwa kuwa Watanzania ambao walitoka ndani ya gari na kukimbia. 

Wankyo amebainisha gari hilo linaonyesha linamililiwa na Uswege Mwamboma wa Tukuyu Mbeya. 

Kamanda huyo aliwataka mmiliki wa gari na ambao wamehusika kuwasafirisha wahamiaji hao haramu kujisalimisha wenyewe kabla hawajatiwa nguvuni.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top