} });
 

 

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ametoa wito kwa vyama vya upinzani nchini kuwa viache ubinafsi kwa kuwa Tanzania ni kubwa kuliko vyama na kwamba Watanzania hawatowasamehe kama hawatoamua kuwa na mgombea mmoja wa Urais, Ubunge na Udiwani. 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 18, 2020, Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa mpaka sasa viongozi wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya vyama hivyo kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao na anaamini kuwa Watanzania wengi wanataka mashirikiano. 

"Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo,na kila Kata, wito wangu kwa viongozi wenzangu wa vyama vya upinzani tuache ubinafsi, Watanzania wanataka ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika nchi, na joto la uchaguzi mmeliona watu wamechangamka Bara na Visiwani" amesema Zitto Kabwe. 

Zitto ameongeza kuwa yeye na chama chake wako tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuweza kuitoa CCM madarakani

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top