} });
 

 

Rais aliyepinduliwa nchini Mali, Ibrahim Boubacar Keita, amesafirishwa kupelekwa Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya matibabu.

Mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa jina lakini anafahamu tukio hilo, amesema hayo na kuongeza kwamba Keita ameondoka akiwa pamoja na Mke wake, Madaktari wawili, Mawakala wanne wa kiusalama na msaidizi.

Jumanne ya wiki hii Keita alipelekwa katika hospitali moja mjini Bamako na kulazwa ambapo hadi siku ya Alhamisi aliporuhusiwa kutoka hospitalini hapo kwa madai kwamba hali yake ya afya ilikuwa inaendelea vizuri.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top