} });
 


Polisi Nchini India inamshikilia mwanaume mmoja wa wilaya ya Badaun nchini humo, Uttar Pradesh, kwa kumjeruhi mke wake ambaye ni mjamzito kwenye maeneo ya tumbo kwa kumrushia upanga kwa madai ya kutaka kujua jinsia ya mtoto.

Kwa mujibu wa familia ya mwanamke huyo wanandoa hao wana watoto watano wa kike na kwamba mwanaume huyo amekuwa akimuhangaisha mke wake amzalie mtoto wa kiume.

Mwanamume huyo ambaye tayari amekamatwa amekanusha madai ya kumshambulia makusudi mke wake akisema ilikuwa ni ajali lakini bado polisi wanaendelea na uchunguzi

Ripoti ya Wizara ya Fedha ya India inabainisha kwamba wanandoa wengi nchini humo wanaendelea kuzaa hadi wapate mtoto wa kiume.

Kila mwaka, watoto wa kike karibu 460,000 wanauawa kupitia utoaji mimba huku vifo vingi vya watoto wa kike wanaozaliwa na kutelekezwa baada ya kuzaliwa vikiripotiwa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top