} });
 


TATIZO sugu la uhaba wa maji katika wilaya nne za mkoani Tanga linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kufuatia Serikali kuwa na mpango wa kutekeleza mradi mkubwa utakaogharimu sh 100. bilioni.

Wilaya zitakazonufaika na mradi huo utakaotoa maji katika mto Pangani ni Pangani,Muheza,Korogwe na Handeni.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amesema hayo wakati wa ziara yake yakukagua miradi ya maji inayosimaniwa na Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Jiji la Tanga Tanga UWASA katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Amesema Kuwa ujio wa miradi hiyo katika mkoa huo utaweza kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji kwa zaidi ya asilimia 90% hali ambayo itasaidia kuimarisha uchumi wa wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa maeneo ya Vijiji ni asilimia 65% wakati katika maeneo ya mjini ni asilimia 18%pekee.

Amesema kuwa ukamilikaji  wa miradi ya maji utaweza kuongeza kiwango cha huduma hiyo hadi kufikia asilimia 52% na hivyo kusaidia kupunguza kwa kiasi fulani Changamoto ya ukosefu wa maji katika wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Jiji la Tanga Tanga UWASA Geofrey Hilly amesema kuwa kukamilika kwa mradi wa maji kutoka Pongwe kwenda Muheza kutasaidia huduma ya maji hadi katika Vijiji vya jirani katika  maeneo ambayo mabomba ya maji yatapita.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top