} });
 

Gari anayotumia mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu imepata ajali eneo la Msoka Kata ya Ngogwa, Jimbo la Masalala mkoani Shinyanga, wakati wakitoka  kwenye mkutano wa Kampeni katika jimbo hilo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, afisa habari wa Chadema Tumaini Makene kupitia ukurasa wake wa twitter amesema gari alilokuwa anatumia mgombea mwenza wa urais Chadema imepata ajali na wote waliokuwa kwenye gari hiyo ni wazima wa afya. 

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwaponya katika ajali hii mbaya wote waliokuwa kwenye gari hii inayotumiwa na mgombe wa kiti cha makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Salum Mwalimu Juma Mwalimu” Tumaini Makene

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top