} });
 


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imemkamata Maria Edson Mtambo (25) Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.12 kuelekea nchini India, dawa hizo alizihifadhi katika kifurushi cha vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa binti huyo ni mfanya usafi huko Tegeta na aliyekuwa anamtumia dawa hizo ni mpenzi wake raia wa nje.

Kaji amewataka vijana kuwa makini na raia wa nchi za Magharibi kwa usalama zaidi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top