} });
 


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limewataka wamiliki wa shule nchini kuhakikisha wanafunga vifaa maalumu vya awali vya kuzimia moto ili kuweza kudhibiti majanga pindi yanapotokea na kupunguza athari za majanga hayo. 

Akiwa katika eneo la shule ya msingi ya Byamungu Islamic iliyoungua moto juzi Septemba 14, mkoani Kagera, Kaimu kamishna wa operesheni wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji, DCF Charo Mangare amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama inaendelea na uchunguzi na pindi itakapokamilisha taarifa itatolewa kwa wananchi ili kuwepo sasa mbinu za kudhibiti ajali kama hizo.

Aidha Kamishna Mangare amewaagiza makamnda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kukagua shule zote kama kuna vifaa maalumu vya kuzimia moto na kusihi zoeli kuwa endelevu ili kudhibiti madhara ya ajali hizo pindi zinapotokea. 

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamishna Mangare Muuguzi Mkuu Msaidizi, Justine Katalaiya amesema majeruhi wanne kati ya sita waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya wilaya ya Karagwe wamehamishiwa Hospitali ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top