} });
 

 

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Sumbawanga Mjini Mkoani Rukwa, Jacob Mtalitinya amesema zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi wanauza kadi zao za kupigia kura kisirisiri.

Amewatahadharisha kuhusu kitendo hicho ambacho ni Kinyume cha Sheria na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Amelazimika kutoa tahadhari hiyo kutokana na taarifa kuwa baadhi ya watu wanapita Nyumba kwa Nyumba na Mtaa kwa Mtaa wakivichukua vitambulisho hivyo baada ya kuwahadaa wamiliki.

Aidha amesema, kampeni zinaendeshwa kwa amani Jimboni hapo na vyama vyote, Vyama vya Siasa ambavyo tayari vimezindua na vinaendelea na kampeni ni CCM, CHADEMA, CUF, ACT-Wazalendo na NCCR-Mageuzi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top