} });
 

John Shibuda akiteta jambo na mama yake mzazi kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha ADA TADEA kitaifa wilayani Maswa

Mgombea Urais kupitia Chama cha ADA TADEA, John Shibuda amesema chama hicho hakina uadui na chama chochote cha kisiasa nchini badala yake maadui wakubwa wa chama cha ADA TADEA ni Ujinga, Umaskini na Maradhi huku vita kuu ya chama hicho ni kuhakikisha utawala bora unapatikana. 

Shibuda amebainisha hayo Septemba 27, 2020 wakati akizindua kampeni za chama hicho kitaifa wilayani Maswa Mkoa waSimiyu ambapo amesema kuwa suala la Umaskini,Ujinga na Maradhi bado ni tatizo kubwa nchini.

“Sisi kama chama cha ADA TADEA hatuna tatizo lolote na vyama vingine vya siasa bali tatizo letu kubwa ni mapambano dhidi ya madhira watatu ambao ni ujinga,maradhi na Umaskini na vita ya chama chetu ni kuhakikisha kuwa utawala bora unapatikana”

Amesema kimejipanga kuondoa maadui wakubwa wa ustawi na maendeleo ya jamii ya watanzania ambapo amewaomba watanzania kumpigia kura ili awezea kuongoza dola.

Katika hatua nyingine Shibuda ametaja vipaumbele vinnne vya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ikiwemo suala la utawala wa sheria wakati wote kwa wananchi na watendaji wa umma sambamba na siasa safi na atawajibika kwa uwazi,ushirikishwaji, uwajibikaji, ufanisi na uadilifu.

Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Magharibi kupitia chama hicho, Lydia Mbuke Bendera amewaomba wakazi wa Maswa kumpigia kura ili aweze kutatua kero ,changamoto na adha mbalimbali ambazo zimeendelea kuwepo ndani ya jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mingi .

Amesema kuwa iwapo atachaguliwa suala la kwanza kushughulikia ni changamoto ya kina mama kusafiri umbali mrefu,kero ya miundombinu pamoja na kumtua ndoo mama kichwani ikiwa ni kusogezwa huduma karibu na wananchi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top