} });
 

 

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Zanzibar wameamua kujitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi badala ya kutegemea mikopo.

Shein ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal III Kisauni, ambapo mesema kuwa mradi huo umelipiwa na fedha za ndani.

“Kwahiyo sasa ndugu wananchi tumeamua tunajitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi lazima tufanye wenyewe hii kukopakopa wakati mwingine tunachelewesha maana mpaka wakubali wenyewe ndo watukopeshe,” amesema Dkt.Shein.

“Lakini tukipanga vizuri bajeti yetu wenyewe tutafanya mambo mengi sana, tumeonyesha njia miaka miwili iliyopita,” ameongeza Dkt. Shein.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top