} });
 

 

Jumla ya mwanafunzi 10 wamekufa kwenya ajali ya moto iliyotokea shule ya msingi Islamic (Byamungu) iliyopo kata ya Itera wilayani Kyerwa, Kagera. 

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mwaimu amethibitisha kutokea kwa ajali ya moto iliyopelekea vifo hivyo na kusema kuwa moto huo umetokea majira ya saa 9 usiku. 

Akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa ni bweni la wavulana,watoto wadogo kati miaka 6-13, watoto 6 wamekimbizwa hospitali huku watoto 3 bado hawajajulikana walipo na wanahofiwa kufunikwa na kifusi kwani bweni limeanguka. 

Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 74.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top