} });
 


Uongozi wa mtaa wa Karume kwa kushirikiana na jeshi la polisi wam+eanza kuwachukulia hatua baadhi ya vijana wafanyabiashara katika soko la Ilala ambao wanalala sokoni hapo mara baada ya kutumia dawa za kulevya pamoja na uvutaji bangi.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Karume kata ya Ilala, Haji Bechina, amesema vijana hao wamekuwa kero si kwa wananchi wanaofika sokoni hapo bali pia hata kwa uongozi wa soko.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko mengi sana kuhusu hawa vijana hivyo kwa sasa tumeanza kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwaondoa kabisa” amesema Bechina

Amesema vijana hao wamekuwa wakichafua taswira ya soko kutokana na vitendo wanavyovifanya ikiwa ni pamoja na uhalifu lakini pia na kuwabugudhi wateja ambao wanafika katika soko hilo kwa ajili ya mahitaji mengine

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top