} });
 

 

Kutoka +254 leo September 11, 2020 Makamu wa (Naibu) Rais wa Kenya, William Ruto amesema Kenya haitashuhudia tena machafuko kwasababu ya Siasa kama ilivyokuwa mwaka 2007.

Akihutubia mkutano wa hadhara Mjini Kisii, Ruto amesema baadhi ya wanasiasa walikuwa wakitumia vitisho kudai huenda kukazuka machafuko mwaka 2022.

Ruto “Wakenya hawatapigana kwa sababu ya Uchaguzi, wajinga hawapo tena. Nchi hii itakuwa na amani na mjue hakuna atakayeshurutishwa kufanya jambo kinyume na hiari yake".

Ruto ameyasema hayo siku mbili tu baada ya Kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwataka Watendaji wa Naibu Rais kutolipeleka Taifa kwenye enzi za giza na machafuko.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top