} });
 

 

Na Imani Anyigulile - Mbeya
Makamu wa rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi Wa mkoa Wa mbeya kuwachagua viongozi wataoweza kuwaletea maendeleo kwa kushirikiana na wananchi katika jamii.

Ameyazungumza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya ambapo amesema kuwa endapo watapata nafasi ya kuchaguliwa watahakikisha wanaboresha miradi mikubwa ikiwa ni pamoja na miundo mbinu ya barabara, maji katika sehemu mbalimbali Mkoani mbeya.

Nae mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Mbeya mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi Tulia Ackson Mwansasu amesema kuwa anawashukuru wananchi wa mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano wa kazi mbalimbali alizozifanya mkoani Mbeya ikiwa ni pamoja na kuboresha secta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara na huduma ya nishati ya umeme hapa jijini Mbeya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa machinga mkoa wa Mbeya Shadrack Mwamwenda amesema kuwa wanamshukuru mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi Dkt. John Magufuli kwa kuwajari wamachinga wa jiji la Mbeya na kuwafanya wafanyebBiashara zao kwa kutulia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top