} });
 

 

Leo September 11, 2020 Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania amefariki dunia usiku wa kuamkia leo September 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha na kusema kuwa Jaji Mstaafu Mzee Bomani alilazwa hospitalini hapo kwa siku 24. 

“Jaji Mstaafu amefia hapa Muhimbili, amefariki majira ya saa 4:00 usiku wa kuamkia leo, na alikuwa hapa hospitalini kwa siku 24” Aligaesha. 

Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole ameandika kupitia Twitter  “Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha Jaji (Mst) Mark Bomani, MwanaCCM & Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, Uongozi unatoa pole kwa familia, wafiwa & wote walioguswa na msiba huu. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top