} });
 

 

Idadi ya watiu waliofariki dunia kutokana na kuporomoka kwa jengo la makazi la ghorofa tatu magharibi mwa India Jumatatu wiki hii imengezeka hadi 20 na miili zaidi inatarajiwa kupatikana chini ya vifusi vya jengo hilo, maafisa wamesema leo Jumanne.

Shughuli za uokoaji zinaendelea ili kupata manusura katika magofu ya jengo hilo lililoporomoka huko Bhiwandi, karibu na mji wa Bombay.

Siku ya Jumatatu, waokoaji kutoka Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Majanga (NDRF) waliweza kuokoa watu 20 wakiwa hai ikiwa ni pamoja na wavulana wawili wenye umri wa miaka minne na saba.

Msemaji wa Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Majanga (NDRF) amewaambia waandishi wa habari kuwa timu za uokoaji, zikisaidiwa na mbwa, walipata miili ishirini katika mabaki ya saruji na vifusi vya matofali ya jengo hilo lililoanguka Jumatatu kabla ya alfajiri.

Mkurugenzi mkuu wa NDRF, Satya Narayan Pradhan, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba wanatarajia kupata miili zaidi kutoka chini ya vifuzi vya jego hilo.

Sababu za tukio hilo hazijajulikana kwa sasa. Maporomoko ya majengo yanaripotiwa mara kwa mara nchini India kati ya mwezi Juni na Septemba, wakati wa msimu wa masika, na mvua kubwa wakati mwingine inasababisha hasara kubwa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top