} });
 


Watu wanne ambao ni Ally Sadick,Anna Kimaro,Tumsifu Kimaro na Steven Kimaro, wamefikishwa mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam wakikabiliwa na makosa matatu ikiwemo la kutishia kuua.

Mashtaka hayo yamesomwa Septemba 22 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Vicky Mwaikambo na wakili wa serikali Ashura Mzava, na kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba, 05, mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka washtakiwa kati ya Agosti mosi na 30,2007 katika eneo la kunduchi mtongani Jijini Dar es salaam wanadaiwa kula njama ya kufanya tendo ovu la kutishia kuua.

Katika shtaka la pili  washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa la kuingia isivyo kisheria katika kiwanja na kujenga nyumba mali ya Mohamed Mshindo.

Inadaiwa kati ya Agosti mosi na 30 2007,washtakiwa walimtishia kumuua Mohammed Mshindo kwa kumwambia "hatutoki hapa,ukifanya masihara tutakuua".

Aidha hakimu Mwaikambo amesema kuwa dhamana iko wazi na mshtakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja anatakiwa kuwa mfanyakazi anayetambulika kisheria na kusaini bondi ya milioni kumi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top