} });
 


Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Hamad ameweka wazi kuwa chama chao kwa upande wa Tanzania bara kitapata majimbo yasiyopungua 30 na hii ni kutokana kazi alioifanya Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe.

Akihutubia umati wa watu uliojitokeza katika mkutano wake uliofanyika Kigoma Maalim ambapo amesema kuwa Zitto amekuwa akifanya kazi kubwa sana zaidi ya punda bila kuchoka. 

"Mimi wakati mwingine nikimwambia kiongozi wangu pumzika lakini yeye ananiambia maalim nitampumzika baada ya kuchukua majimbo na mimi naamini kwa kazi aliyoifanya Zitto inshaallah tutapata majimbo yasiyopungua 30 mwaka huu hiyo  kwa Tanzania bara tu." alisema Maalim.

Aidha Maalim aliendelea kumsifia kiongozi huyo kwa jinsi anavyojali Watanzania na kusema, "√úzuri wa Zitto sio tu kwamba anatetea Kigoma, anatetea masikini wote Tanzania, "Zitto ni mtoto wenu anaipenda sana Kigoma lakini Zitto ni mwana wa Tanzania anayeipenda sana Tanzania huyo ndio kiongozi"

Hata hivyo Maalim ameupongeza uongozi wote wa Kigoma kwa kazi nzuri walioifanya na Halmashauri ya Kigoma mjini kuwa ni nzuri kwa Tanzania

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top