
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kumtia mbaroni mtu anayeshukiwa kuwa
jambazi Luka Kavishe wa kijiji cha Mbomai wilayani Rombo kwa kuhusika na mauaji ya kikatili
ya marehemu Febronia Mangowea wa kijiji hicho miaka mitatu iliyopita.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro kamishna msaidizi wa Polisi Emmanuel Lukula
amesema, mauaji hayo yalifanyika julai 31 mwaka 2017 saa moja na nusu usiku katika shamba
la marehemu katika kijiji hicho na kukamatwa mwaka huu katika eneo la kata ya pasua
manispaa ya Moshi.
Kamamda Lukula amesema, kabla ya kifo chake marehemu alibakwa kinyama na mtuhumiwa
kwa imani za kishirikina ambazo kamanda amezikemea na kueleza kuwa hazihusiani na
mambo ya ushirikina.
Mtoto wa Marehemu Bi.Teddy Tesha amewapongeza polisi wa vituo vya Tarakea, mkuu Rombo
na Moshi mjini kwa ushirikiano nzuri uliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa ambaye
alitoroka baada ya mauaji hao miaka mitatu iliyopita.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment