} });
 


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ametoa onyo kwamba yeyote ambaye anasema atamwaga damu mkoani humo, yeye anataka lita saba za damu yake, na ameongeza kwamba wanaotaka kufanya maandamano, viongozi wao wawe mstari wa mbele.

 

Amesema hayo mara baada ya kumaliza kupiga kura leo katika uchaguzi mkuu na ameeahakikishia wananchi usalama  kamili ili wajitokeze kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

 

 “Niendelee kuwasisitiza, leo kama ni maandamano basi naomba viongozi wao, nipo chini ya magoti yao, viongozi ndiyo wawe mbele, ili kama ni kufyatua basi wafyatuliwe vizuri.

 

“Ukimaliza kupiga kura nenda kanywe bia, wanaosema watakaa kulinda kura wala msiwe na wasiwasi nao, hivi ukiweka pesa zako benki unakaa hapohapo benki kuzilinda?” alisisitiza.

 

Aidha, kuhusu mitandao kutofanya kazi, amesema ni kawaida mitandao kusumbua na yeye hana taarifa ya maandishi ya mitandao kutoweka hewani kwa sababu ya uchaguzi.

 

Ameongeza kuwa kuna mgombea alidai mawakala wake hawajaapishwa na kuwa atavaa mabomu kuingia barabarani na damu itamwagika.

 

“Sitaogopa mbunge, wala diwani, kabla hajaingia barabarani atakuwa ameshasambaratishwa, kama ni ulemavu leo nitaanza na viongozi wao, huyo anayesema anamwaga damu, akithubutu mimi nitataka lita saba za damu yake,” amesema Chalamila.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top