} });
 

 

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi amewahidi Wazanzibar kuwa serikali yake ikingia madarakani  itahakisha bandari mpya ya mafuta na gesi itajengwa eneo la Bumbwini Mkoa wa Kaskzini Unguja.

Dkt.Hussein Mwinyi ametoa ahadi hiyo alipokuwa akizumgumza na wanachama wapezni wa Chama cha Mapinduzi na wakazi wa Bumbwini Mkoa Wa Kaskazini Unguja Oktoba 07, 2020 na kusema mradi huo umeshaanza na utakamilishwa na serikali yake. 

Mgombea Urais huyo wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar pia amezungumzia suala la ajira kwa vijana, ambapo suala la viwanda na uvuvi ndiyo  nguzo zake muhimu za kuziendeleza na kuzisimaamia. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top