
Na Imani Anyigulile - Mbeya
Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Mbeya kupitia mgombea wake Joseph Mbilinyi kimefanya mkutano wake katika kata ya Ituha huku akieleza aliyo yafanya katika jimbo hilo na kile anacho tarajia kukifanya kipindi cha miaka mitano.
Joseph Mbilinyi amesema kuwa akiwa mbunge amehimiza maendeleo kwa kuboresha huduma za afya sambamba na kutetea maslahi ya watumishi wa umma.
Kwa upande wa elimu amesema kuwa ametoa misaada mbalimbali kupitia mfuko wa jimbo.
Katika hatua nyingine mgombea wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amefanya mkutano katika kata ya Iyela na kusema kuwa hiki ni kipindi cha kutoa hesabu na sikutafuta kura za huruma kwani serikali ya chama cha mapinduzi imejipanga na imefanya mengi kupitia elimu ya msingi na sekondari.
Post a Comment