} });
 


Polisi mjini Philadelphia wamesema mamia ya wezi wamevamia na kuiba kwenye maduka ya biashara katika usiku wa pili wa ghasia zilizozuka baada ya polisi kumpiga risasi na kumuua mtu mweusi.

Polisi wa ziada pamoja na walinzi wa kitaifa wamepelekwa katika mji huo kutuliza ghasia. Maafisa wanasema polisi 30 wamejeruhiwa katika usiku wa kwanza wa ghasia hizo.

Polisi wanasema walimpiga risasi Walter Wallace, 27, alipopuuza amri ya kumtaka aangushe chini kisu alichokuwa ameshikilia mkononi.

Familia ya Bw. Wallace inasema alikuwa anakabiliwa na tatizo la afya ya kiakili.

Usiku wa Jumanne, polisi waliwaonya wenyeji kusalia ndani ya nyumba zao na kujiepusha na maeneo ya Riverfront Port Richmond kwasababu watu wamekuwa wakiiba katika maduka ya watu.

Ofisi ya Philadelphia ya kushughulikia hali ya dharura iliwashauri wakazi kusalia ndani kwasababu kulikuwa na "maandamano makubwa ambayo yamegeuka kuwa ya ghasia".

Kwa mujibu wa maafisa mjini Philadelphia, waandamanaji walijaribu kuweka vizuizi barabarani kwa kutumia vifaa vya kuzolea taka.

Polisi walilazimika kutumia maji ya kuwasha na fimbo kuwatawanya waandamanaji lakini walishambuliwa na waandamanaji hao.

Maduka katika mji huo yalifungwa mapema lakini yalivunjwa vio na mali kuibiwa usiku wa Jumanne.

Meya Jim Kenney, wa chama cha Democratic, amesema kanda ya video inayoonesha jinsi polisi walivyompiga risasi na kumuua mtu mweusi siku ya Jumatatu "inazua maswali magumu ambayo lazima yajibiwe".

Meya huyo hakutoa ufafanuzi zaidi, lakini alisema anatazamia " uchunguzi utafanywa haraka kubaini kwa uwazi kilichotokea kwa niaba ya Bw. Wallace, familia yake, maafisa waliohusika na wenyeji wa Philadelphia".

Kamishna wa polisi wa Philadelphia Danielle Outlaw amesema kwamba amefika katika eneo la tukio na alikutana na "Jamii iliyokuwa imejawa na hasira ".

"TunataraJia kushuhudia ongezeko la visa vya ghasia," alisema katika mkutano na wanahabari mapema Jumanne . "Naongeza kwamba tutachukua hatua zaidi kuhakikisha hali ya utulivu unadumishwa. Tutaongeza idadi ya maafisa wetu katika maeneo muhimu mjini."

Maandamano makubwa yaliibuka mapema mwaka huu kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi mjini Minneapolis, Minnesota

Kanda ya video iliyosambazwa mitandaoni ikimuonesha afisa wa polisi mzungu Derek Chauvin akipiga goti kwenye shingo ya Bw. Floyd kwa dakika kadhaa licha ya mtu huyo kurudia kusema hawezi kupumua.

Kifo cha Floyd kilisababisha maandamano makubwa kote duniani kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi.

Zaidi ya watu 300 walimiminika barararani kupinga Kauai ya Bw. Wallace na 91 kati Yao walikamatwa.

Maandamano halo yaliendelea hadi alfajiri ya Jumanne yalikubwa na vurugu mara kwa mara.

Picha kutoka eneo la tukio zilionesha jinsi gari la polisi lilivyochomwa moto na mane kadhaa ya biashara kuvamiwa na kuibiwa.

Afisa mmoja alivunjwa mguu naw engine kushambuliwa kwa vifaa butu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top