} });
 


Mahakama moja nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi inayohusisha wanaume watatuwalioshtakiwa kwa kusaidia wanamgambo wenye silaha kushambulia jengo la manunuzi katika mji mkuu wa Nairobi, mwaka 2013.

 

Takriban watu 67 waliuawa katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika jumba la manunuzi la Westgate.

 

Wanamgambo wa Kiislamu wenye makao yao nchini Somalia walikiri kutekeleza shambulizi hilo. Aidha serikali ilisema kwamba wanamgambo waliotekeleza shambulizi hilo waliuawa.

 

Zaidi ya watu 140 walitoa ushahidi kwenye kesi hiyo ambapo washitakiwa walikanusha kufanya njama ya kutekeleza ugaidi.

 

Kutolewa kwa hukumu kutahamasisha nchi ambayo bado ipo katika tahadhari ya juu kwa uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la kigaidi, na ambayo jeshi lake bado liko nchini Somalia kukabiliana na vikosi vya al-Shabab kutoka kwenye kambi zao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top