} });
 


HUENDA mashabiki wa soka nchini Uingereza wanaweza kurejea tena viwanjani hivi karibuni, baada ya ombi la mashabiki kupata saini nyingi kutoka kwenye Bunge la Uingereza ambalo limepanga kuijadili taarifa hiyo Novemba 9, mwaka huu.

 

Tangu mwezi Machi serikali ilipiga marufuku mashabiki kuingia viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona, hivyo hatua hiyo endapo itafikiwa ni nafuu kwa vilabu vingi ambazo vinategemea zaidi mapato ya mlangoni kuendesha klabu zao.

 

Licha ya kuchezwa bila ya mashabiki, ligi hiyo imeendelea licha ya ukweli kuwa imepungua msisimko na ladha, ambapo mpaka sasa zimechezwa raundi nne.  Timu ya  Everton inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 12 wakishinda mechi zote  nne walizoshuka dimbani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top