} });
 

 

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije ametaja orodha ya Wachezaji wa timu ya Taifa ambao wataingia kambini Oktoba tano mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi ndani ya Uwanja wa Mkapa Siku ya Okatoba 11.

Kikosi hicho kinaundwa na Makipa, Metacha Mnata (Yanga SC), Aishi Manula (Simba SC) na David Kisu (Azam FC); Mabeki ni pamoja na Nickson Kibabage (Difaa El Jadida – Morocco), Shomary Kapombe (Simba SC), Israel Mwenda (KMC FC), Mohammed Hussein (Simba SC), Brayson David (KMC FC), Bakari Mwamnyeto (Yanga SC), Abdallah Sebo (Azam FC), Dickson Job (Mtibwa Sugar) na Iddy Mobbi (Polisi Tanzania).

Kwa upande wa Kiungo, Stars itaundwa na Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (ENPPI SC – Misri), Feisal Salum (Yanga SC), Ally Msengi (Stellenbosch FC – Afrika Kusini), Said Hamis “Ndemla” (Simba SC), Mzamiru Yassin (Simba SC) na Salum Aboubakar “Sure Boy” (Azam FC).

Washambuliaji katika kikosi kitaongozwa na nahodha, Mbwana Samatta (Fenerbahce – Uturuki), Wengine ni Simon Msuva (Difaa El Jadida – Morocco), Ditram Nchimbi (Yanga SC), John Bocco (Simba SC), Iddy Nado (Azam FC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo)

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top