} });
 


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema hadi sasa wananchi wengi wamekuwa watulivu licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wachache walioandaliwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kufanya vurugu na kujiingiza kwenye uhalifu. 

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kuwataka baadhi ya viongozi kufanya masuala ya siasa na kuacha kuwatumia vijana na kuwaingiza kwenye uhalifu na kwamba yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Kuhusu upigaji wa kura Zanzibar, IGP Sirro amesema, wapo baadhi ya watu wanaohamasisha baadhi ya watu au kikundi cha watu kuvunja sheria wakatiwa zoezi la upigaji kura kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top