} });
 

Jeshi la uhamiaji mkoa wa Mwanza limewakamata wahamiaji haramu 24 kutoka nchi za Burundi na Rwanda kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria na taratibu waliokutwa wakifanya kazi katika kanisa la Baba Godi lililopo eneo la Kangae ‘A’ wilaya ya Ilemela jijini Mwanza pamoja na viongozi saba wa kanisa hilo ambao ni raia wa Tanzania wanaotarajiwa kukishwa mahakamani.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Bahati Mwaifuge amesema Jeshi la uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi walifika katika kanisa hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kuwakamata watu hao.  

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top