} });
 

 

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,(CCM), Dkt. John Magufuli, amesema kuwa mgombea aliyeongoza katika kura za maoni jimbo la Kawe Furaha Dominic, ni mtoto wa dada yake, lakini aliamua kukata jina lake na kumchagua Mchungaji Gwajima, kwani hawezi kushindana naye.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 9, 2020, katika mkutano wa kampeni wa chama hicho kwa Jiji la Dar es Salaam, wakati akijiombea kura na kuwaombea kura wagombea udiwani na ubunge ndani ya jiji hilo.

"Naomba niwaambie huyu ni Askofu ni mkweli sana, na ndiyo maana nataka niwaeleze ukweli, aliyeongoza kura za maoni Kawe ni mtoto wa dada yangu, nilimkata jina kwa sababu hawezi akashindana na Gwajima, wa Kawe naomba wamlete Gwajima akajime kweli kweli", amesema Dkt. Magufuli.

Aidha Dkt.Magufuli akaoneshwa kushangazwa na mgombea urais aliyeshangaa upana wa barabara ya Kimara hadi Kibaha, "Hii barabara ya Kimara, Kibaha nilisikia mgombea wa urais akilaumu kwamba tunajenga barabara pana na kwamba ametembea nchi nyingi hajawahi kuona, majibu yake ni kwamba si kweli kwamba barabara hii ni pana kuliko zote Duniani".

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top