} });
 

 

Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi, amemwaga sera zake kwa wananchi wa jimbo hilo, na kuahidi endapo wakimchangua kuwa mbunge wao atahakikisha anakuza uchumi wa wakulima na wafugaji.

Katambi amenadi sera zake Oktoba 0, 2020 kwenye mkutano wa kampeni eneo la Soko kuu la mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wananchi, mgombea udiwani wa Kata ya Mjini Gulam Mukadam, wanachama wa chama hicho wakiwamo na viongozi, waliongozwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa. 

Alisema kwa utafiti walioufanya Jimbo la Shinyanga mjini, halina wafugaji wa kutosha ambao wataweza kuhudumia kiwanda cha nyama pamoja na machinjio ya kisasa, na kuahidi wananchi endapo wakimchagua kuwa mbunge wao Oktoba 28 mwaka huu, atatenga eneo kubwa kwa ajili ya kufugia mifugo tu na kuinua uchumi wa mfugaji. 

“Mimi nataka kiwanda hiki cha nyama ambacho tutakifufua, pamoja na machinjio ya kisasa iliyopo, malighafi yake ambayo ni ng’ombe itoke kwa wazawa ambao ni wana-Shinyanga wenyewe ili muinuke kiuchumi,” alisema Katambi. 

Pia alisema kwa upande wa kilimo, ataleta taasisi ya utafiti ya kilimo (Tari), ili kubaini mbegu za kilimo ambazo zinakubalika maeneo ya Shinyanga, ili wananchi walime kilimo chenye tija ambacho kitawainua kiuchumi, na siyo kufanya kilimo cha kubahatisha. 

Katika hatua nyingine aliahidi kuboresha mazingira ya wafanyabiasha, ikiwamo kulikarabati Soko kuu la mjini Shinyanga, kuvutia wawekezaji, pamoja na wafanyabishara wa usafirishaji wakiwamo baiskeli za daladala, bodaboda, na bajaji, kuwapatia mikopo kupitia vikundi ili wapate kupanuka kibiashara. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, aliwataka wakazi wa jimbo la Shinyanga mjini siku ya kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu wasifanye makosa bali wamchangue Katambi, pamoja na mgombea Urais John Magufuli, ili wawaletee maendeleo na Shinyanga iendane na uchumi wa kati.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top