
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Bw.Tundu Lissu anaendelea na harakati zake za kusaka ridhaa ya kuingia Ikulu katika uchaguzi mkuu wa utakaofanyika tarehe 28 mwezi huu.
Leo (jana) mgombea huyo alikuwa katika Kijiji cha Iguguno, Wilaya ya Mkalama jimbo la Iramba
Mashariki Mkoani Singida, ambako mgombea huyo wa Urais ameahidi kuwa na sheria
zitakazolinda uhuru kamili wa kutoa maoni kwa vyombo vya habari, bunge pamoja na
kuboresha miundombinu ya barabara za vijijini pindi akipewa ridhaa ya kuingia ikulu ya
chamwino.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Bwana Oscar Kapalale akiomba kura katika Kijiji cha Nduguti Wilayani Mkakama, ametaja baadhi ya matatizo mbali mbali yanayokwamisha harakati za maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo iliyoanzishwa Julai Mosi mwaka 2013.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment