} });
 

 

Naibu katibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Avemaria Semakafu amesema serikali imefuta mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi na awali kwa ngazi ya cheti na badala yake mafunzo yataanzia ngazi ya Stashahada (Diploma).

Amesema hayo leo Oktoba 5, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa wizara imefanya maboresho ya mtaala wa ualimu wa awali na shule za msingi ambayo itatolewa kwa kipindi cha miaka mitatu na mafunzo ya cheti hayatotolewa tena.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefuta mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi na awali kwa ngazi ya cheti, badala yake mafunzo yataanzia ngazi ya Stashahada (Diploma)“ amesema Semakafu.

 “Walimu wenye vyeti waliopo makazini wasiwe na wasiwasi hakuna mtu atakayeondolewa kazini, haya ni maboresho tu na wataelekezwa namna ya kujiendeleza endapo wakihitaji kufanya hivyo” amesema Semakafu.

Naye mkurugenzi Taasisi ya Elimu, Dkt. Aneth Komba amesema kuwa walimu wa shule za msingi waliokuwa wanahamia shule za sekondari walipelekea upungufu wa walimu katika shule za msingi.

Aidha amesema kuwa maboresho hayo ya mataala yasaidia kupata maprofesa na Madaktari walimu wa shule za msingi na awali.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top