} });
 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameongoza mapokezi ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mapokezi hayo, yamefanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar leo tarehe 02 Oktoba, 2020 ambapo Mhe. Dkt. Magufuli ameeleza kwa ufupi.

“Leo nimeingia hapa Zanzibar, nimeingia Zanzibar kwa ajili ya kuja kufanya Kampeni, kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi.”

Mgombea wa Urais wa CCM Mhe. Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa kampeni kesho tarehe 3 Oktoba, 2020 katika viwanja vya Mnazi mmoja Mkoa wa Mjini.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top