} });
 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania amesema, hakumfukuza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Magufuli ameeleza hayo ameyasema hayo akiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha Mjini leo Oktoba 23 wakati akinadi wagombea mbalimbali Mkoani humo.

Magufuli amesema kuwa, kama angemfukuza asingelipitisha jina lake (Gambo) Halmshauri Kuu ili awe Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM.

Juni 19 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ambapo siku chache baadaye Gambo alitangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini.

Magufuli yupo mkoani Arusha akiendelea mkutano wa Kampeni za Chama za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki ijayo, Oktoba 28.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top