} });
 


Mahabusu ambaye alikuwa na kesi ya mauaji, Musa Haji Mchana, alipigwa na radi na kupoteza uhai Oktoba 13 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ukanda wa Pwani.

Aidha wafungwa wanne wamejeruhiwa na radi hiyo na hivi sasa wako hospitali wakiendelea na matibabu. Wafungwa hao ni Richard Simau, Issa Haji, Hashim Rashid na Ismail Mtupa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema gereza lililopata kadhia hiyo ni gereza la Wilaya linaloitwa Mng’aro lililoko Kibiti.

Kamanda amesema hakuna wafungwa wala mahabusu waliotoroka baada ya kupigwa na radi hiyo na ulinzi umeimarishwa zaidi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top