} });
 


Watu wanne ambao ni mawakala wa CHADEMA, wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, katika ajali ya gari iliyotokea leo Oktoba 21, 2020 kijiji cha Malonji, Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Justine Masejo, amethibitisha na kueleza kuwa watu watatu wamefariki hapohapo na mmoja amefariki akiwa hospitali.

Aidha ACP  Masejo amesema kuwa majeruhi wanaendelea na matibabu akiwemo dereva ambaye yupo chini ya ulinzi.

Ameongeza kuwa gari iliyopata ajali ni Noah yenye namba za usajili T 381 DZQ, huku chanzo kikiwa ni ugeni wa dereva kwenye barabara hiyo na aliendesha gari kwa kasi hivyo ikamshinda kwenye kona na kupelekea ajali.

Zaidi msikilize kamanda hapo chini

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top