} });
 


Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Saashisha Mafuwe, ameibuka mshindi katika Jimbo la Hai katika uchaguzi uliofanyika jana Jumatano, Oktoba 28, 2020.


Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Yohana Elisha, amemtangaza kuwa Mafuwe amepata kura 89,786 huku mpinzani wake Freeman Mbowe wa Chadema akipata kura 27,684 na wa tatu ni Mbaruku Mhina (ACT) mwenye kura 315.


Hivyo Mafuwe ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Hai na kumburuza Mbowe aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top