} });
 


Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anatarajiwa kuwasili nchini kesho kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa na mechi ya kifariki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi itakayochewa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Samatta ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya ushindi ya Fernebahce dhidi ya Fatih Karagumluk katika mechi ya ligi kuu nchini Uturuki iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ikumbukwe timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars inaingia kambini leo Oktoba 5 huku baadhi ya wachezaji walioitwa na kocha Etienne Ndayiragije wamewasili kambini kujiwinda na mchezo huo. 

Wachezaji wengine wa kimataifa ni pamoja na Thomas Ulimwengu anayetarajiwa kuwasili leo akitokea Congo DR, Himid Mao, Simon Msuva na Nickson Kibabage kutokea Misri na Morocco watawasili Jumatano naye Ally Msengi tayari amewasili akitokea Afrika Kusini.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top