} });
 

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Salome Makamba kwa tuhuma za kufanya fujo, kuchana karatasi za matokeo ya kura na kumjeruhi Msimamizi wa Uchaguzi katika kituo cha kuhesabia kura cha Shule ya Msingi Bugweto “B”.

 

RPC wa Shinyanga, Magiligimba amethibitisha kumshikilia mgombea huyo; “Baada ya matokeo kukamilika kujumlishwa, alipewa karatasi ya matokeo kuyasoma, nadhani hakuridhika nayo aliamua kuichana karatasi ya matokeo hayo na kumshambulia msimamizi wa uchaguzi katika kituo hicho na kumjeruhi mguu….”

 

“Hivyo tunamshikilia kwa ajili ya upelelezi, ukikamilika tutamfikisha mahakamani. Sisi Jeshi la Polisi Shinyanga tumejipanga kwa yeyote atakayetaka kuleta virugu au uvunjifu wa amani tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria,” amesema Magiligimba.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top