
Watu watano wa familia moja akiwemo mama, watoto wake watatu pamoja na wi yake
wamepoteza maisha baada ya nyumba yao kuwaka moto majira ya saa nne usiku wa kuamkia
leo katika eneo la Pugu CCM Kirumba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mahojiano maalum baba wa familia hiyo Edward katemi
amesema moto huo ulianza majira ya Saa nne usiku na waliofariki katika familia hiyo ni Mke
wake Jackline Frank, mdogo wake Ester Katemi na watoto wake Edwin Katemi, Edson katemi
pamoja na Evon Katemi.
Bw.Edward amesema kwa kushirikiana na majirani zake walipambana kuiokoa familia yake bila
mafanikiko kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuwezesha uokoaji katika tukio hilo na
waliwasiliana na watu wa kikosi cha uokoaji lakini walichelewa kuka kutokana na changamoto
ya usari iliyokuwepo.
Kamanda wa polisi Ilala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema watu hao walifanikiwa
kuokolewa na kukimbizwa hospitali lakini kwa bahati mbaya walipoteza maisha na chanzo cha
moto bado hakijafahamika japo moto huo ulianzia sebuleni.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment