} });
 


Siku chache baada ya kuifyatua Manchester United mabao sita kwa moja, meneja wa Totenham Hotspurs Jose Mourinho, amesema haikuwa rahisi kufanikisha ushindi huo mkubwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mourinho amesema imekua faraja kwake kushinda mchezo huo kwa idadi kubwa ya mabao, kwani katika Ligi ya England miongoni mwa timu ngumu kuzishinda ni Manchester United.

Amesema mchezo dhidi ya magwiji hao wa England huwa na mazingira magumu na yenye kutatanisha, na wakati mwingine huleta mijadala kwa mashabiki wa soka duniani kote.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno amesema: “Moja ya timu ngumu kucheza nazo ndani ya England ni pamoja na Manchester United,  ni ngumu kucheza nao na kupata ushindi kwa uhakika ndani ya dakika 90, hasa kwenye uwanja wa Old Trafford.

“Ugumu wake ni kwamba unaweza ukawashinda ndani ya uwanja baada ya dakika 90 lakini huwezi kupata furaha ya kushangilia huo ushindi mpaka ufike nyumbani kwa kuwa unaweza kushangaa upo ndani ya chumba cha kubadilishia nguo mwamuzi anakufuata na kukwambia mwambie kipa wako ajiandae Bruno Fernandes anakwenda kupiga penati.

Mabao ya Spurs kwenye mchezo huo uliomalizika kwa mchezaji wa Manchester United Anton Martial kuonyeshwa kadi nyekundu yalifungwa na Tanguy Ndombele, Heung-Min Son, Erik Lamela, Heung-Min Son, Serge Aurier na Harry Kane aliefunga mabao mawili huku bao la wenyeji likifungwa na Bruno Fernandes.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top